MATANGAZO


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, April 11, 2011

TUBADILI MAZINGIRA (LET'S CHANGE OUR ENVIRONMENT

Ndugu wapendwa wanajamii wenzangu, hasa kwa nchi yetu ya Tanzania.  Ninapenda sana tuzungumzie habari ya mazingira kwani siri ya mafanikio yote kimaisha huanzia kwenye Mazingira.  Mungu ametupa nchi nzuri ya kupendeza lakini tumeshindwa kuitunza mpaka tunayachukia mazingira yetu na kutamani mazingira ya nchi zingine.  Jamani hivi ni kweli tumeshindwa kutunza mazingira yetu?????  Mimi bado naona hatujashindwa ila ni vile tu hatujaamua kufanya hivyo. 

Ndugu zangu napenda mjue kuwa mazingira yetu ndio siri pekee inayoweza kubadili hata hali halisi ya maisha yetu na kuwafanya hata wengine watamani kujifunza toka kwetu. Jamani usafi wa mazingira huanzia kwako mwenyewe, Jikoni, maliwatoni (vyooni), mazingira yanayozunguka nyumba yako nk.  Kweli ukiweka mazingira yako yakiwa safi mwenyewe utapenda kuwepo nyumbani kwako.  Usafi unakufanya uwe na afya njema na pia huleta furaha daima.

Ikumbukwe kuwa hakuna mtu atakayeleta mabadiliko ya maisha yako isipokuwa ni wewe mwenyewe.  Anza leo kutamani mazingira yako yawe na mvuto wa tofauti.  Usisubiri kuona jirani anafanya nini.  Wewe fanya kwanza na wengine watakufuata.  Tumeharibu sana mazingira yetu kiasi kwamba hata hewa tunayovuta hutusababishia magonjwa. Lakini bado muda tunao na tunaweza kufanya kila kitu kiwe kwenye hali ya kawaida (everything can change back to normal).
Hebu tazama picha hizi upate kujifunza zaidi.



 Je? unapoishi katika mazingira kama haya utaepuka kupata magonjwa ya mlipuko?